Ukaribisho
Dkt. JUMA R. JUMA
MGANGA MFAWIDHI
KARIBU HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SONGWE KWA HUDUMA BORA ZA MATIBABU.HOSPITALI YA RUFAA INATOA HUDUMA MBALIMBALI ZA MATIBABU IKIWEPO HUDUMA ZA KAWAIDA NA HUDUMA ZA KIBINGWA.HOSPITALI INA HUDUMA 7 ZA KIBINGWA IKIWEMO HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MAGONJWA YA MASIKIO,PUA NA KOO,MAGONJWA YA WANAWAKE NA UZAZI,MAGONJWA YA MACHO,MAGONJWA YA WATOTO,MAGONJWA YA AFYA NA MAGONJWA YA AKILI,MAGONJWA YA DHARURA,MAGONJWA YA NDANI.
PIA HOSPITALI INATOA HUDUMA ZA KLINIKI ZA KAWAIDA IKIWEMO KLINIKI YA KINYWA NA MENO,KLINIKI YA BABA,MAMA NA MTOTO(RCH),KLINIKI YA VIUNGO NA MAZOEZI TIBA,KLINIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA KISUKARI NA PRESHA NA KLINIKI YA CTC(KIFUA KIKUU NA HIV).HOSPITALI INA WATUMISHI WA KUTOSHA AMBAO WANATOA HUDUMA KWA UBORA KWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KITATBIBU.PIA HOSPITALI INATOA HUDUMA ZA VIPIMO VYA MAABARA KWA KUPIMA SAMPULI KWA MASHINE ZA KISASA NA UPANDE WA DAWA TAASISI IMEWEKEZA ASILIMIA 99.9 KWA KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA DAWA KWA WAGONJWA.
PAMOJA NA HAYO,ASANTENI KWA KUCHAGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SONGWE KAMA KITUO BORA CHA MATIBABU,NA HOSPITALI INAAHIDI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA ILI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.