UVCCM Mbozi washirikiana na Viongozi wa Songwe RRH katika zoezi la kupanda miti.

Posted on: February 6th, 2023

Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya mbozi mkoa wa Songwe wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbozi Cde, Nelson Joseph Mwakyusa. wameshirikiana na Viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe kwenye zoezi la kupanda miti katika mazingira ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbozi Cde, Nelson Joseph Mwakyusa amekiri kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya Afya wilaya ya Mbozi.

Pia amepongeza sana Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania.